Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, na kulia ni mtia nia wa nafasi ya Urais, Lazaro Nyalandu.
Nyalandu ametoa kauli hiyo hii leo Julai 8, 2020, wakati akichukua fomu ya kuomba uteuzi wa chama ili aweze kupewa ridhaa ya kuipeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao na kusema kuwa CHADEMA watakapoingia madarakani, watakuwa wako tayari kukosolewa muda wote bila kumuathiri mkosoaji.
"Mwaka 2000 tulikuta na Mh Mbowe, wakati fulani nikiwa CCM na yeye CHADEMA nilimuambia tusafiri katika maeneo ya Wapalestina na Waisrael, na tukaenda Yerusalemu saa 6 usiku tukaenda katika ukuta wa maombolezo na sala Mbowe aliandika na mimi nikaandika ya kwangu, sasa sijui aliandika siku moja niende CHADEMA, lakini ninaufahamu moyo wake na kupitia yeye chama kimeweza kusimama katika nyakati za mitihani na majaribu" amesema Nyalandu.

