Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kulia ni Balozi Mstaafu Job Lusinde wakati wa uhai wake.
Rais Magufuli ametoa salamu hizo za pole, kupitia ukurasa wake wa Twitter hii leo Julai 8, 2020,
"Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Balozi (Mst) Job Lusinde, nawapa pole familia, wana Dodoma na Watanzania, nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na Kiongozi wa Wazee wa Dodoma, Pumzika salama mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri" ameandika Rais Magufuli.
Balozi Mstaafu Job Lusinde, alimefariki Dunia Alfajiri ya Julai 7, 2020, katika Hospitali ya Mloganzila na mipango yote ya mazishi inafanyika nyumbani kwake jijini Dodoma. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Balozi Lusinde, mahali pema Ameen.



