Friday , 12th Jun , 2020

Mwandishi wa kujitegemea wa EATV katika mkoa wa Songwe, Manuel Kaminyoge amefariki dunia leo jioni katika hospitali ya Ikonda mkoani Iringa alipokuwa anapatiwa matibabu.

Manuel Kaminyoge

Kaminyoge alihamishiwa katika hospitali ya Ikonda baada ya kupewa rufaa kutoka Songwe kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kupata ajali wiki tatu zilizopita.

Kwa mujibu wa Kaka wa marehemu, Musa Kaminyoge, mipango ya mazishi inaendelea kufanyika mkoani Songwe. 

Uongozi wa EATV unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.

Pumzika kwa amani Manuel Kaminyoge.