Friday , 17th Oct , 2014

Wahitimu mbalimbali wa kozi ya Ukocha nchini wametakiwa kutumia elimu wanayoipata ili kuweza kupata vijana wenye vipaji vipya watakaoweza kuitangaza nchi katika michezo ndani na nje ya nchi.

Bonifase Mkwasa

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mratibu a kozi ya wanamichezo wa kamati ya Olimpiki nchini TOC iliyochini ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Boniface Mkwasa amesema Tanzania inahitaji walimu wa michezo wa kutosha katika soka na haina maana yoyote iwapo watamaliza mafunzo na kuacha kutumia elimu waliyoipata.

Mkwasa amesema wahitimu hao watawezeshwa kwa ajili ya kuendeleza vituo vyao vya michezo ili kuweza kuviboresha zaidi.