
Mpira rasmi wa Premier League msimu wa 2019/20
Taylor amesema kuna uwezekano mkubwa pindi ligi itakaporejea mapumziko yakawa sio dakika 45, ili kuwapa nafasi wachezaji kuendelea kurejea kwenye hali ya kawaida.
''Wakati tunafikiria kurejea kwa ligi ni muhimu kuwaangalia wachezaji pia, wana maisha pia, juu ya usalama wao na kama wanaridhika pia kurejea uwanjani na ndio maana ni muhimu kujiridhisha ikiwemo kuwapa nafasi zaidi ya kupumzika'', amesema Taylor.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Premier League Rick Parry yeye amesema hawajajadili chochote kuhusu hilo ila inawezekana wakafanyia kazi kwasababu katika kipindi hiki hawatapuuzia pendekezo lolote lenye manufaa.
Ligi kuu ya England ilisimamishwa rasmi tangu Machi 13, kupisha janga la Corona lakini sasa inatarajiwa kurejea muda wowote ndani ya mwezi Juni.