Sunday , 3rd May , 2020

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kushangazwa kufuatia sampuli za Papai, Mbuzi kukutwa na Virusi vya Corona baada ya kupimwa kwenye Maabara kuu ya Taifa.

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Magufuli amesema hayo wakati akimuapisha Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba Chato mkoani Geita, ambapo amemtaka kwenda kufanya uchunguzi kwenye suala la maabara ya Taifa.

"Tulipeleka Sampo ya Ndege Kware ilikuwa Positive, Mbuzi akawa Positive, Kondoo akawa Negative, ukishaona sampo ukamwambia huyu ni binadamu halafu ana Corona maana yake Mapapai yote yangewekwa Isolation" amesema Rais Magufuli

"Tulipopeleka sampo ya Papai tukaipa jina la Elizabeth (26) Papai lile lilikuwa Positive kwamba lina Corona, maana yake maji ya Papai ni Positive." ameongeza Rais Magufuli