Sunday , 3rd May , 2020

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na mchumba wake Carrie Symonds, wametangaza kumpa mtoto wao wakiume jina la Wilfred Lawrie Nicholas Johnson, ikiwa jina kati la Nicholas ni la madaktari waliomtibu Waziri huyo ugonjwa wa Corona.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na mchumbwa wake Carrie Symonds

Mtoto huyo ambaye amezaliwa siku ya Jumatano ametangazwa kupewa jina hilo jana Mei 2,2020, huku jina hilo ni ishara ya heshima kwenda kwa madaktari waliomtibu Waziri ugonjwa wa Corona wakati alipoumwa ugonjwa huo. 

Akizungumza kwenye akaunti binafsi ya mtandao wa Instagram mchumba wa Waziri wa Uingereza Carrie Symonds amesema  "Jina la Wilfred ni baada ya babu wa Boris, Lawrie ni baada ya Babu yangu, na Nicholas ni kwa heshima ya Madaktari waliomsaidia kumtibu Corona Boris ambao ni Dr. Nick Prince na Nick Hart

Waziri huyo anatarajia kurejea kazini Jumatatu ya Mei 4,2020 baada ya kuwa kiongozi wa kwanza mkubwa duniani kutangazwa kuwa ana virusi vya ugonjwa wa Corona mnamo mwezi Machi.

Chanzo : CNN