Wednesday , 15th Apr , 2020

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza ongezeko la wagonjwa 29 wa COVID-19 ambapo wote ni Watanzania, 26 wapo Dar es Salaam, wawili wapo Mwanza na mmoja yupo Kilimanjaro, hali inayopelekea Tanzania kuwa na jumla ya visa 88.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema kuwa ongezeko hili la wagonjwa linajumuisha wagonjwa wapya sita, waliotolewa taarifa na Waziri wa Afya wa Zanzibar leo Aprili 15, 2020.

Aidha wagonjwa waliopona wamefikia 11, huku vifo navyo hapa nchini Tanzania vikifikia vinne.