Tuesday , 10th Mar , 2020

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga, amewajia juu mashabiki wa Yanga, baada ya wao kutoa kauli za kwamba Simba wamewaoa, kitendo ambacho kinaonesha udhalilishaji  kwa wanawake na ili hali kuolewa si kushindwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Anna Henga ameandika hayo leo Machi 10, 2020, Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ikiwa imepita siku moja tu tangu timu ya Yanga, ilipoipa kichapo cha goli timu ya Simba, katika mchuano wake wa mpira wa watani wa jadi.

"Hongera sana mashabiki wa Yanga, hata hivyo naomba lugha inayotumika isiwe ya kudhalilisha jinsia ya kike!, unaposema Simba kaolewa au Yanga kaolewa unamaanisha kuwa kuolewa ni kushindwa (kufungwa), kwa kawaida anayeolewa ni Mwanamke! maana yake ni nini? #Aminiausawa" ameandika Anna Henga.