Tuesday , 25th Feb , 2020

Siku ya Februari 24, 2020 katika viwanja vya Staples Center, Los Angeles nchini Marekani, palifurika maelfu ya watu kusherehekea kumbukumbu ya maisha ya Kobe Bryant na mwanaye wa kike Gianna Bryant, ambao walifariki kwa ajali ya helicopta siku ya Januari 26,2020.

Picha ya marehemu Kobe Bryant enzi hizo akicheza kwenye timu yake ya LA Lakers

Katika hafla hiyo walijitokeza mastaa mbalimbali wakiwemo Kanye West, Kim Kardashian, Beyonce, Snoop Dogg , Alicia Keys, Jennifer Lopez, Alex Rodriguez, Michael Jordan, Steph na Ayesha Curry.

                                 Picha ya mke wa Kobe Bryant aitwaye Vanessa Bryant

Sasa moja ya vitu vilivyotokea kwenye shughuli hiyo ni staa wa Pop duniani Beyonce kukataa kupigwa picha alipokuwa anaimba wimbo wa XO na Halo kama heshima ya mwisho kwa Kobe Bryant.

                 Picha ya msanii Beyonce akiwa anaimba katika kumbukumbu ya maisha ya Kobe Bryant

Mkongwe wa mchezo wa Basketball Michael Jordan, kumwaga machozi hadharani wakati akielezea ukaribu aliokuwa nao na Kobe Bryant.

                  Mkongwe wa mchezo wa Basketball Michael Jordan akitokwa na machozi 

Pia katika uwanja huo wa Staples Center, ndipo mahali walipoagwa na kutolewa heshima za mwisho kwa mkali wa muziki wa pop Michael Jackson na rapa Nipsey Hussle.

                              Uwanja wa Staples Center mahali ambapo shughuli hiyo imefanyika

Wawili hao tayari walishazikwa siku ya Februari 7,2020 katika makaburi ya Pacific view memorial park jijini California.