Thursday , 2nd Oct , 2014

Mchekeshaji mahiri wa nchini Kenya, Eric Omondi amechaguliwa kuwa balozi wa hifadhi ya Lake Nakuru huko Kenya ambapo moja ya majukumu yake itakuwa ni kupigania utunzaji wa wanyama jamii ya kiboko ambao ipo mbioni kupotea.

mchekeshaji nyota wa nchini Kenya Eric Omondi

Kazi hii mpya ya Eric katika sekta ya Utalii na hifadhi ya mali asili, ni mkakati maalum kuhakikisha vifaru wapatao 70 waliobakia katika hifadhi hii wanabaki katika mikono salama kwa kusambaza taarifa sahihi juu ya jukumu la kila mwananchi juu ya ulinzi wao.

Taarifa za uteuzi wa Eric katika nafasi hiyo zimetolewa rasmi huko nakuru, katika shughuli maalum ya uhifadhi ya wanyama hawa ambayo kwa mwaka huu imefanyika kwa awamu ya 10.