Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa, Halima Mdee
Halima Mdee ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo ameitaka Serikali kuleta mabadiliko ya Sheria ya Ndoa Bungeni ilikufanyia marekebisho.
"Kati ya watoto 5 wawili wanaolewa chini ya miaka 18, na wengi wao wanachukuliwa kuanzia miaka 8 mpaka 10 na hakuna anayechukua hatua, ndiyo maana ni kawaida kusikia Mwalimu kabaka wanafunzi wake 24" amesema Halima Mdee
"Kutokana na alilolianzisha Mwanaharakati Rebeka sisi BAWACHA tunaitaka Serikali kuleta mabadiliko ya Sheria ya Ndoa, ili kumnusuru mtoto wa kike" ameongeza Mdee
"Kati ya watoto 5 wawili wanaolewa chini ya miaka 18, na wengi wao wanachukuliwa kuanzia miaka 8 mpaka 10 na hakuna anayechukua hatua, ndiyo maana ni kawaida kusikia Mwalimu kabaka wanafunzi wake 24" - @halimamdee - Mwenyekiti BAWACHA#BAWACHAPress pic.twitter.com/1wAiPXejVt
— East Africa Radio (@earadiofm) January 8, 2020

