Tuesday , 7th Jan , 2020

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amesema kabla ya kifo cha Mama Mzazi wa Mwandishi wa habari Erick Kabendera, Verdiana Mujwahuzi, alihudhuria Mahakamani mara 2, licha ya kuwa ni mgonjwa.

Zitto Kabwe amesema kifo cha Mama huyo ni moja ya vifo, ambavyo vimegusa idadi kubwa ya Watanzania, kutokana na namna ambavyo Erick Kabendera alikuwa akiishi vizuri na watu.

Zitto Kabwe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mazishi ya Mama Mzazi wa Erick Kabendera, yaliyofanya jana Januari 6, 2020, katika Kijiji cha Kashenge, Kata ya Katoma Bukoba Vijiji, mkoani Kagera.

"Katika kesi mbili za mwisho ambazo Erick alikuwa mahakamani, Mama alikuja, tulimlaumu Dada yake Rose kwanini alikuwa anamleta Mama, kumbe mama alikuwa anamuaga Mwanae" amesema Zitto.

Mama wa Erick Kabendera alifariki Dunia siku ya Disemba 31, 2019, katika hospitali bya Amana iliyoko jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.