Saturday , 4th Jan , 2020

Msanii Billnass amesema hana lolote la kuongea baada ya kuona picha tata za Nandy akiwa na Ommy Dimpoz ambazo walipiga wakati wanashoot video ya wimbo wao.

kushoto ni Billnass, kulia ni Ommy Dimpoz akiwa na Nandy katika moja ya picha iliyozua gumzo

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, kuhusu kuona picha za picha za Nandy  Billnass amesema, hayupo sana kwenye maadili  ila  yupo katika upande wa uandishi, utunzi, hiphop na kufanya show.

"Zile sio picha zangu mimi ajibu mtu mwenye picha zake, sipo sana kwenye maadili nipo kwenye utunzi, uandishi, hiphop na kufanya show suala la maadili kuna baraza wanaweza kuzungumza zaidi, nafanya video kila siku nashoot kwa watu na warembo tofauti na hii ni tasnia ambayo vitu vyote vinavyofanyika navijua" ameeleza Billnass

Aidha Billnass ameachia Comment kwenye picha ya Nandy baada ya kuona picha hizo ambapo ameandika "Haaaa eeeh Mungu tuvushe mpaka mwezi Juni".

Picha za Nandy na Ommy Dimpoz  ambazo zimepostiwa katika kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram zimezua gumzo mitandaoni kutokana na mapozi na mavazi ya picha hizo.