
Picha Kushoto ni Msanii Alikiba na Kulia ni Muigizaji Lucy Okoth anayedai kuwa na mahusiano naye.
Taarifa hizo zilisambaa katika mitandao ya kijamii, siku ya Disemba 17,2019, baada ya muigizaji huyo, kufanya mahojiano na chombo kimoja cha habari kilichopo jijini Nairobi, na kusema kuwa anazo tattoo 10, huku mojawapo ikiwa na jina la Alikiba.
"Nina tattoo kama 10 mwilini mwangu, sijawahi kujutia kuzichora, bado nina mchoro wenye jina la mpenzi wangu wa zamani Ali Kiba, kamwe siwezi kujutia kuwa naye kwenye mahusiano, siwezi kumsahau kwenye asilimia 70 ya maisha yangu, pia alikuwa na mahaba kwa asilimia 100" amesema Bridget Achieng.
Kwa upande wa Alikiba mwenyewe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa wimbo mpya wa Chaku, alioshirikishwa na Christian Bella ameeleza kuwa.
"Suala la kunichora tattoo nalipokea kama shabiki yangu, sio yeye peke yake kuna wengi tu ambao wamechora na nishaonaga zamani sana ile tattoo na suala kuwa na mahusiano na mimi ilo hapana sio kweli" amesema Alikiba.
Alikiba anaendelea na ziara yake ya Kimuziki mkoani Iringa, aliyoipa jina la AlikibaUnforgettable Tour, ambapo siku ya Disemba 21, 2019, atawakutanisha wana Iringa katika viwanja vya Samora, kuanzia saa 12 jioni, akiwa na wasanii wengine kama Tundaman, Christian Bella na kundi la Kings Music.