Wednesday , 18th Dec , 2019

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Baraza la Vyama na Vilabu Afrika Mashariki na Kati CECAFA kwa kipindi cha miaka 4 ijayo.

Rais mpya wa CECAFA, Wallace Karia

Karia amechaguliwa katika nafasi hiyo leo kwenye Mkutano Mkuu wa CECAFA uliofanyika nchini Uganda, ambapo atakuwa akisaidiana Makamu wa Rais wawili ambao ni Francis Amin kutoka Sudan ya Kusini na Esayas Jiro wa Ethiopia.

Rais wa TFF amezungumza baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo pamoja na vitu atakavyovifanya kwenye nafasi yake, ambapo amesema atasimamia vizuri katika upatikanaji wa wadhamini, kuimarisha michuano ya soka la ufukweni pamoja na kusimamia nchi wanachama na waalikwa wanashiriki kikamilifu kwenye michuano inayoadaliwa na baraza hilo.

Pia katika mkutano huo imeshuhudiwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka na Vilabu Afrika Mashariki na Kati CECAFA, Nicholas Musonye akiachia ngazi katika nafasi yake hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka 20.