
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Makonda ameyabainisha hayo leo, Disemba 18, 2019, wakati alipotembelea kukagua miundombinu iliyoharibiwa na mvua na kuwataka wananchi wanaokaa maeneo hatarishi wahame, kwani ipo siku wao wanaofanya maombi hayo ya kumbembeleza Mungu watazidiwa nguvu.
"Jana ilibidi tufanye kazi kubwa ya kuwasiliana na Mungu na kumbembeleza ili mvua leo isiwepo, leo angalau Jua limewaka hivyo tuitumie hii nafasi tuende sehemu salama na si wote wanaomuomba Mungu akakubali jambo, itakuja kunyesha Mvua ya siku tano tutapoteana hapa mjini, hivyo watu wa mabondeni hameni, sasa tunaombembeleza Mungu apunguze hii mvua itafikia mahala tutazidiwa uwezo" amesema Makonda.
Hata hivyo Makonda amesema Serikali kwa sasa inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa Mito na Mifereji kwa lengo la kupunguza kero ya mafuriko kwa wananchi, ambapo kwa Wilaya ya Ilala kuna ujenzi wa Mito yenye urefu wa Km 16, Temeke Km 14 na Kinondoni Km 8 ili maji yaende moja kwa moja baharini.