Monday , 16th Dec , 2019

Wizara ya Elimu imewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), kuwa watulivu na kuendelea na masomo, wakati tamko lao walilolitoa kwa Bodi ya Mikopo likiendelea kushughulikiwa, ambapo Bodi hiyo imesema kwasasa inawasiliana na uongozi wa chuo hicho ili kulijadili kwa pamoja

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

na baadaye leo kulitolea ufafanuzi.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Disemba 16, 2019, Mkuu wa Mawasiliano wa Bodi hiyo Omega Ngole, amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni wadau wao wakubwa hivyo watalishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.

"Tumeliona hilo tamko na hivi tunawasiliana na uongozi wa Chuo Kikuu kulipatia ufafanuzi ambao tutautoa baadaye leo na mimi binafsi nimelisoma na sisi kama Taasisi ya Umma, kikitokea kitu kama hicho tunakifanyia kazi, maana Chuo Kikuu ni wadau wetu muhimu sana katika utoaji wa mikopo" amesema Ngole.

Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho, imetoa masaa 72 ikiitaka Bodi yaMikopo, kumbadilisha Afisa Mikopo chuoni hapo, kuwalipa mikopo yao wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao rufaa zao zimetupiliwa mbali, pamoja na kurudisha fedha zote za wanafunzi zilizokatwa.