
Askari wakifanya shughuli ya kuokoa miili ya marehemu
Tukio linatajwa kutokea saa saba usiku wa kuamkia Disemba 16, 2019 katika Kata Nsemulwa mkoani Katavi, ambapo inasemekana majambazi hao walivamia nyumba hiyo na kuwauwa wapenzi hao.
Akizungumzia tukio hilo Dada wa Marehemu Noel Mswanya, Joyce Mswanya "nimepigiwa simu saa 12 : 30 usiku na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, kuwa mdogo wangu Noel ameshauawa, na nilimkuta wifi yangu na yeye ameuawa akiwa nje ya nyumba"
"Naomba sana Serikali isaidie kuwatafuta wahusika wa tukio hili ili ikiwezekana wakamatwe wachukuliwe hatua za kisheria" ameongeza Joyce mswanya
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Katavi bado zinaendelea.
#HABARI Noel Mswanya na Stela kisanga ambao ni Mume na Mke wakazi wa Mtaa wa Nsemulwa wilayani Mpanda mkoani Katavi, wameuawa kwa kukatwa mapanga, baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo. pic.twitter.com/r7QoyZ2Nly
— East Africa TV (@eastafricatv) December 16, 2019
Tazama mahojiano ya Dada wa marehemu hapo chini