Saturday , 14th Dec , 2019

EATV & EA Radio Digital imepiga stori na msanii wa kike Wini Tz, ambaye amesema kama kuna mwanaume yeyote anayejiamini na anasema amemnunulia gari ajitokeze amuone.

Msanii Wini

Wini Tz amesema hayo baada ya kuwepo na taarifa zinazosema gari analotumia aina ya "Harrier Lexus" amehongwa na mwanaume wala hajanunua kwa pesa zake mwenyewe.

"Mishe zangu ni kupambana kama mtoto wa kike, nasimama kama mimi bila kumtegemea mwanaume yeyote yule, kwa hiyo nilipambana kwa mihangaiko ambayo nimeifanya kama Wini, kupitia muziki wa "live band" na kilimo changu ndipo nilipo jibariki na kitu kama kile" amesema Wini Tz.

Aidha msanii huyo ameongeza kusema "Kwa hiyo kama kuna mwanaume ambaye anaamini yeye kanunua lile ndinga aje hapa au nyinyi mleteni yule mnaemjua nyinyi, wasichana tunaweza sio mpaka uwe na miaka 80 huko au 90 ndiyo ununue gari, sikuhizi vijana tunapambana tunatakiwa tubadilishe akili zetu" ameongeza.

Pia amesema hawezi kuwahukumu  wanawake wanaotumia njia fupi  ili kutengeneza maisha yao, wala hawezi kuwashauri wafanye vibaya,  na hawezi kudhibiti nafsi za watu, kila mtu anayetamani kufanya vitu vyake afanye ila kwa njia iliyo salama.