Wednesday , 24th Sep , 2014

Msanii wa muziki Cindy Sanyu, amepoteza tena haki ya malezi ya mwanae Amani katika mapambano ya kisheria dhidi ya baba wa mtoto huyo na mpenzi wake wa zamani, Mario Brunett.

msanii wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu

Kwa mujibu wa maamuzi ya hakimu Rose Jolly Onyango ambaye alikuwa akisikiliza shauri hili, Cindy ameonekana kutokutosheleza vigezo vya kutoa malezi bora ya mtoto huyu kama ambavyo Mario ameonyesha.

Kwa sasa Cindy ameonekana kukolea katika mahusiano na mpenzi wake mpya, Ken Muyiisa ambaye tayari amekwishakumtambulisha nyumbani kwao, wakiwa na mpango wa kufunga naye ndoa.