Kushoto ni Gadiel Michael wa Taifa Stars na kulia ni wachezaji wa Kilimanjaro Queens.
Ijumaa timu ya taifa ya soka ya wanaume itakuwa dimbani kwenye uwanja wa taifa, kuivaa Equatorial Guinea, katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 nchini Cameroon. Mchezo huo utaanza saa 1:00 usiku.
Kwa upande mwingine timu ya taifa ya soka ya wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens itaanza kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la CECAFA, ambapo itafungua dimba na Sudan Kusini, mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Chamazi Dar es salaam.
Tayari timu za taifa kutoka mataifa shiriki zimeanza kuwasili nchini, ambapo timu za Taifa za Wanawake za Djibouti, Burundi na Kenya tayari zimeshawasili nchini tayari kwa michuano hiyo.
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Kenya imewasili Tanzania tayari kwa michuano ya CECAFA kwa Wanawake inayotarajia kuanza Novemba 16 mpaka Novemba 25,2019 Dar es salaam #cecafa2019motoniuleule @WKidao @azamtvtz @Football_Kenya pic.twitter.com/IDYRJNbOq1
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) November 13, 2019
Michuano ya CECAFA kwa Wanawake inatarajia kuanza Novemba 16 mpaka Novemba 25,2019 Dar es salaam. Kilimanjaro Queens ndio mabingwa watetezi wakiwa wametwaa mara mbili mfululizo.