Wednesday , 17th Sep , 2014

Sakata la kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe imechukua sura Mpya baada ya Wajumbe wa bunge maalum la Katiba wanaounda umoja wa Tanzania Kwanza kuwataka wapenda amani kuungana pamoja kulaani kauli zilizotolewa na mwenyekiti huyo.

Mbunge wa jimbo la Sikonge nchini Tanzania Mh. Saidi Nkumba.

Kauli hiyo ni ile anayodaiwa kutoa wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Mlimani City ambapo Mwenyekiti huyo anadaiwa kutoa tishio la kuandamana kudai kusitishwa kwa bunge maalumu la katiba

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma mwenyekiti wa kundi la Tanzania kwanza, ambaye pia ni mbunge wa Sikonge, Said Mkumba amesema kauli hizo sio tu zinachochea vurugu bali pia zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Amesema wao Tanzania Kwanza wanalaani kwa nguvu zote kauli hizo na kwamba mchakato wa kupata Katiba mpya unaendeshwa kwa hoja siyo kwa chuki binafsi wala kwa kuwapotosha wananchi, na kueneza uhasama na kupiga vita katiba yenye maslahi kwa jamii.