Thursday , 11th Sep , 2014

Msanii wa muziki anayefanya shughuli zake katika kundi la P Unit kutoka Kenya, Gabriel Kagundu maarufu kama Gabu, ameingia rasmi katika kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Saratani nchini Kenya.

msanii wa kundi la P-Unit nchini Kenya Gabu

Msanii huyu mwishoni wa wiki hii anatarajia kushiriki katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa 1,000 wa Saratani huko Meru, ambapo amewataka mashabiki na wadau kumuunga mkono katika hili.

Gabu ameeleza kuwa, ameguswa kuingia katika harakati za kupambana na ugonjwa huu kutokana na rekodi kuonyesha kuwa, Saratani ndiyo inayoongoza kwa kusababisha vifo vingi duniani kuliko magonjwa kama Ukimwi, TB na Malaria.