Monday , 2nd Sep , 2019

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Athumani Kihamia, ameshangazwa na kauli  ambayo si ya kweli iliyotolewa na  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, baada ya kugoma kumuapisha diwani aliyeteuliwa na Tume hiyo, kwa madai ya kwamba hajapokea barua ya uthibitisho,

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Athumani Kihamia

inayompa mamlaka ya kumuapisha diwani huyo.
 

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital leo Septemba 02, 2019, Dkt Kihamia amesema kuwa, barua waliyomuandikia Mkurugenzi wa Ubungo, ilijibiwa siku tatu kabla ya kikao cha madiwani na ilisainiwa na Mkurugenzi mwenyewe.

''Barua tuliyowapa Manispaa ya Ubungo waliipokea na walitutumia barua ya kukiri kama wamepokea  siku tatu kabla ya Mkutano wa madiwani wa Halmashauri hiyo na ilisainiwa na Mkurugenzi mwenyewe, kusema kuwa hajapokea barua kutoka kwetu si kweli labda wana mambo yao tu'', amesema Dkt Kihamia.

Jumamosi ya Agosti 31, madiwani wa Ubungo kutoka CHADEMA, waligoma ndani ya kikao kilichokuwa kimeitishwa, wakihisi kufanyiwa mchezo mchafu na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,  baada ya kukataa kumuapisha diwani, ambapo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano  wa  CHADEMA Tumaini Makene, alimtaka Mkurugenzi huyo  kuhakikisha anaondoa vikwazo na kumuapisha diwani wao.