Thursday , 29th Aug , 2019

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema wizara yake inafanyakazi kubwa kwa kusisimia fedha zaidi ya Trillioni 6 kwenye bajeti kuu ya serikali.

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo.

Jafo ameyasema hayo jijini Dodoma kwenye mahojiano Maalum na EATV&EA Radio Digital, juu ya masuala mbalimbali yanayosimamiwa na Wizara yake ikiwemo Elimu, Afya na Miundombinu.

''Wizara yetu ndio yenye dhamana kubwa zaidi na kila mwaka kwenye bajati inatengewa zaidi ya shilingi Trilioni 6, hivyo tuna jukumu kubwa la kuzitumia vizuri kama tunavyofanya hivi sasa kwa kuboresha Elimu, Vituo vya Afya pamoja usimamizi wa Uchaguzi wa serikali za Mitaa'', amesema Jafo.

Zaidi Tazama Video hapo chini.