Sunday , 25th Aug , 2019

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Serikali ya Tanzania haitavumilia taasisi yeyote ambayo itaonesha nia ya kukwamisha zoezi la kuwarejesha wakimbizi, wanaotokea nchi jirani ya Burundi.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Kigoma alipotembelea kambi ya Wakimbizi Nduta, iliyopo wilayani Kibondo mkoani humo akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Burundi.

Waziri Lugola amesema kuwa "wakimbizi wa Burundi wanaoishi Tanzania, wanalelewa vizuri sana na mpango wa Serikali ni kuwarejesha nyumbani kwao Burundi, kwa kuwa sasa kuna amani."

Aidha akieleza nia hiyo Waziri Lugola amesema Serikali katika kila wiki itakuwa ikiwarudisha wakimbizi ili 2000 mpaka pale watakapoisha.