
Taifa Stars dhidi ya Harambee Stars
Safari hii ni katika kuwania kufuzu michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani, ambapo Taifa Stars itawakaribisha Harambee Stars leo jioni katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo, klabu ya soka ya Simba imeahidi kutoa kiasi cha Shillingi milioni 10 kwa wachezaji na benchi la ufundi endapo wataibuka na ushindi katika mchezo huo.
Kazi kwenu @taifastars_ kutupa furaha. Zawadi ya Tsh. 10 Milioni ipo kwa ajili yenu. #NguvuMoja pic.twitter.com/AxToTtNjbY
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) July 27, 2019
Baada ya mchezo huo, Stars itasafiri hadi Nairobi kucheza mchezo wa marudiano na timu itakayoshinda hapo itakuwa na uwezekano mkubwa wa kuvaana na Sudan.