Tuesday , 23rd Jul , 2019

Tunda afunguka usiyoyajua kuhusu uhusiano
Video vixen wa muziki wa BongoFleva Tunda, amefunguka kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na msanii wa muziki na mchekeshaji Whozu, kwa kusema kuwa walikuwa wanafahamiana tangu shule ya msingi, pia nyumbani kwao ni majirani.

Tunda amaefunguka hayo kupitia eNewz ya EATV baada ya kuulizwa kuhusu uhusiano wake na Whozu, wakati alipokuwa anasheherekea siku ya kuzaliwa akiwa ana timiza miaka 23.

Hukohuko kwa kina Whozu ndio kwetu ni majirani, Whozu kwao ni Moshi na sisi kwetu ni Moshi hata nyumbani kwetu tayari wanamfahamu, yaani Whozu alipokulia, shule aliyosoma na mimi  hivohivo, Whozu nimeanza kumfahamu tangu shule ya msingi na tulisoma shule moja Moshi kabla sijahamia Morogoro”. amesema Tunda

Aidha Tunda amesema anatamani kufika mbali na mpenzi wake huyo, sababu anampenda sana anatamani adumu naye, waonane na wawe na familia.

Penzi la Tunda na Whozu limekuja kwa kasi sana na limekuwa likizungumziwa na watu wengi sana kupitia mitandao ya kijamii. Mrembo huyo amewahi kuwa kwenye mahusiano na wasanii na watu wengine maarufu kama Yound Dee na Casto Dickson.