
Christian Bella
Kupitia DADAZ ya East Africa Television Bella amesema anapokea simu zote zinazoingia labda asiwe tu na muda au yupo studio anarekodi.
''Huwezi kujua ni simu ya aina gani inapigwa, inaweza kuwa ndugu yako anaumwa au mtu anataka kukuepusha na janga fulani, ila inakata sana pale shabiki anapokupigia tu analeta stori nyingi au kukuomba uongee na watu wake na wewe huna muda unalazimika kukata'', amesema.
Bella pia ameeleza kuwa moja ya starehe zake kubwa ni kucheza 'Play Station' anapokuwa nyumbani peke yake hususani kwasasa ambapo familia yake ipo Ulaya.
''Starehe yangu kubwa ni 'Play Station' yaani huwa nashinda nacheza nikiwa nyumbani. Starehe yangu nyingine ni kuwa studio, yaani nikiwa pale hata kama mwingine anarekodi mimi napata mzuka wa kuandika au kufanya chochote'' - Christian Bella.