Tuesday , 2nd Sep , 2014

Msanii wa muziki Saraha ambaye anafanya kazi zake za muzik nchini Sweden, amezungumzia ujio wake mpya kupitia kazi inayokwenda kwa jina 'Shemeji' ambayo inatangaza utamaduni na muonekano wa kitanzania, licha ya asili yake ya kizungu.

msanii wa bongofleva nchini Tanzania Saraha

Saraha amesema kuwa video ya kazi hii mpya ameifanyia hapa hapa Tanzania kupitia muongoza video Ray Kasoga huku akitumia madansa na mavazi yaliyobuniwa pia Tanzania, licha ya kazi hii kutengenezwa nje ya nchi.