Watoto wakiwa na sahani za chakula. ( Picha hii haihusiani na habari )
Hali ambayo inaelezwa kuwa inahatarisha afya za watoto na kutishia kushusha kiwango cha ufaulu katika mkoa huo.
Wakizungumza na www.eatv.tv, Mwenyekiti wa kitongoji cha Kilimilile, Iss-Haka Yunus amesema kuwa wananchi walipokuwa wakipata mavuno ya kutosha walikuwa wanajitoa kuchangia mahindi lakini kwa sasa hawana kitu, huku mmoja wa wakazi wa kitongoji hicho Nujibu Ibrahim akiwahimiza wananchi wenzake kujitajidi kuchangia mahindi kwa ajili ya watoto wao.
Aidha Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Sanura Khamis amesema kuwa pamoja na uhaba wa chakula uliopo bado baadhi ya wazazi hawana moyo wa kushirikiana na serikali kuchangia mahindi kwa ajili ya watoto wao kupata uji shuleni.
"Wewe kama mzazi, mtoto wako anakula saa 3 usiku na asubuhi anaamka anakwenda shuleni wewe unabaki nyumbani unapika unakula, mtoto anarudi nyumbani saa 8 biila kula, unakuwa humtendei haki", amesema Afisa Mtendaji wa kijiji hicho.
Naye Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera, Aloyce Kamamba amebainisha mipango iliyopo ya kuhakikisha watoto wote wanapata uji au chakula shuleni ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
"Tumekubaliana kama mkoa na nimetoa maelekezo kwa walimu wakuu kwamba ifikapo tarehe 31 mwezi Machi, wanafunzi wote wawe wanapata chakula mashuleni", amesema Aloyce.
Tazama video hapa chini.