Thursday , 21st Feb , 2019

Baada ya Chid Benz kusema kuwa Jux anabebwa na siyo msanii mzuri, Jux ameibuka na  kusema siku akikutana na Chid Benz uso kwa uso halafu akamuambia hayo maneno ndo atakapomjibu.

Jux

Akiongea kupitia eNewz, Jux amesema kwamba hajasikia chochote ambacho Chid Benz amepanga na anamchukulia Chid kama kaka yake na popote atakapokutana naye ataendelea kumuheshimu kama kaka yake kwa kuwa hajawahi kuona akimvunjia heshima wakiwa pamoja tangu amemfahamu.

"Maneno yameongelewa mengi sana na siamini kama kuna wasanii ambao hawapendi mafanikio yangu kwa mfano Chid Benz  ni mtu ambaye tunaheshimiana sana na nimeambiwa na watu wengi kwamba ameongea kwamba mimi ninabebwa siwezi kukasirika kwa kuwa Chid ni mtu ambaye haniogopi ananiambia chochote hivyo kama kuna tatizo kati yetu naamini akikutana na mimi ataniambia 'live" aliongea Jux.

Lakini pia Jux amemalizia kwa kusema kwamba collabo yake na Nyashinski ni  kubwa sana ambayo amewekeza pesa yake nyingi na kusema sababu ya yeye kuifanyia Video Nairobi ni kutokana na maeneo aliyokuwa anayawaza ambayo mwanzoni ilitakiwa kuwa Afrika ya Kusini.