![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2019/02/08/Janjaaro.jpg?itok=89Fz-9nX×tamp=1549612096)
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende 'Dogo Janja', akiwa na mpenzi wake Linna.
Kupitia kurasa wake wa Instagram Janjaro amefunguka kuwa hakuna neno linaloweza kutosha kuelezea hisia zake kwa mwanadada huyo, ambaye alikuwa akimtumia salamu za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
"Hakuna neno linaloweza kutosha katika kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu mengine nitakuelezea chumbani. Kula ushibe, Kisha kaza chaga nakupenda sana", ameandika Janjaro.
Dogo Janja alionekana na mwanadada huyo siku za hivi karibuni lakini kila alipohojiwa hakutaka kuweka wazi juu ya uhusiano wao.