Saturday , 16th Aug , 2014

Msanii wa Maigizo na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steve Nyerere amesema kuwa, katika uongozi wake, amefanya jitihada kubwa kufungua milango kwa wasanii chipukizi wenye maadili kuingia katika tasnia hiyo.

Steve Nyerere - Rais Bongo Movie Unity

Steve Nyerere amesema kuwa, amekwishaongea na wasanii wenzake wakubwa kutengeneza njia kwa wasanii wadogo, hatua ambayo pia itasaidia kutengeneza kizazi kipya cha wasanii wenye maadili.

Steve Nyerere amesema kuwa, njia hii ya kufungua milango kwa Chipukizi itasaidia kuwajenga wasanii katika misingi ya kujiheshimu na hivyo kukabiliana na changamoto ya uhuni na ugomvi katika tasnia ya Bongo Movie.