
Esperance wakishangilia ubingwa wao.
Simba ambayo inaiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo inakabiliwa na kazi hiyo, haswa baada ya kauli ya Rais Magufuli wakati anawakabidhi ubingwa wa ligi kuu bara, kuwa anataka kuona ikileta ubingwa wa Afrika nyumbani.
Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani (Stade Olympique de Rades), Esperance walifanikiwa kumaliza ukame wa mechi 10 kwenye ligi ya mabingwa bila ushindi dhidi ya Al Ahly kwa kushinda mabao 3-0 na kukamilisha ushindi wa mabao 4-3.
Fainali hiyo huchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ambapo katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Misri wiki moja iliyopita Al Ahly walishinda kwa mabao 3-0 lakini wakashindwa kulinda ushindi wao kwenye mchezo wa jana usiku.
Simba tayari wameshapangiwa timu ya kuanza nayo kwenye hatua za awali za michuano hiyo msimu wa 2018/19 ambapo watakipiga na Mbabane Swallows kati ya Novemba 27 na 28 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa.