
Wachezaji wa taifa Stars
Ndimbo ameiambia www.eatv.tv kuwa mshambuliaji Shabaan Chilunda anayecheza katika klabu ya Tenerife ya Hispania atawahi kujiunga na kambi kuliko wachezaji wengine wa kimataifa.
''Wachezaji wetu wa kimataifa akiwemo Chilunda wataanza kuripoti kuanzia leo Novemba 10, 2018 huku wengine watatu wakitarajiwa kuingia Jumapili Novemba 11, 2018 na Msuva na wengine huenda wakachelewa'', amesema.
Aidha Ndimbo amewataja wachezaji watakaoripoti Novemba 11 ni pamoja na nahodha msaidizi Himid Mao anayecheza Misri, Hassan Kessy anayecheza Zambia, Abdi Banda na Rashid Mandawa.