
Adam Salamba kushoto na Eliud Ambokile
Wachezaji hao wametajwa miongoni mwa majina 38 ya wachezaji wanaounda kikosi hicho chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Morocco.
Hemed Morocco, amesema timu hiyo itacheza mchezo wa kuwania kufuzu AFCON kwa vijana dhidi ya Burundi, mchezo utakaopigwa Novemba 14 na kurudiana Novemba 20 Jijini Daresalaam, huku akiahidi kubakiza wachezaji 25 katika kikosi kabla ya mechi hizo.
Wachezaji wengine walioitwa katika kikosi hicho ni pamoja na Kelvin Sabato wa Mtibwa sugar, Paul Godfrey wa Yanga, Habibu Kiyombo wa Singida United huku Mbao fc wakitoa wachezaji wawili katika kikosi hicho, Hussein Kassanga na mlinzi wa kushoto Amos Charles.
Kikosi hicho kitaingia kambini muda wowote tayari kwa kuanza maandalizi na kumpa nafasi kocha Morocco kuchuja wachezaji watakaomfaa kutoka 38 hadi 25 ambao atasafiri nao kwaajili ya mchezo huo.