
Sindano za kushonea
Kwa mujibu wa matokeo ya X-ray iliyofanywa katika mwili wake, sindano hizo zimeonekana kunasa katika sehemu za moyo, shingo, mikono yake yote pamoja na kwenye utumbo.
Licha ya sindano hizo kuwepo katika mwili wake, mwanamama huyo ameshindwa kutaja ni kwa namna gani zimeingia na kwa muda gani zimekuwepo katika mwili wake.
Inaelezwa kuwa mwanamama huyo alichukuliwa na kupelekwa sehemu isiyojulikana ambako alibakwa, kudhalilishwa na kutupwa porini, alikaa huko kwa kipindi fulani kabla ya kurejea huku akiwa na matatizo ya akili pamoja na kushindwa kumudu matamshi.
"Sisikii maumivu sehemu zingine za mwili isipokuwa katika tumbo langu ambapo ndiyo maumivu makubwa yalipo", amesema Thabita.
Kwa mujibu wa maelezo yake, Thabita alilelewa na mama mmoja ambaye hakuwa mzazi wake kabla ya kuamua kuingia mitaani. Wazazi wake hawafahamu, na hata ndugu zake aliwafahamu baada ya kuolewa na mwanaume aliyemtaja kwa jina la 'Timothy Njenga'.