
Mwanadada Wema Sepetu.
Katika mkutano wake na wanahabari, Wema amesema kuwa kuanzia sasa anafunga jalada la maisha yake ya utoto na kuomba radhi kwa watanzania kutokana na kusambaa kwa picha zake zisizokuwa na maadili mitandaoni.
"Naomba radhi ndugu zangu, jamaa na marafiki na wote waliokuwa wakinisapoti kwa moyo mmoja, na mama yangu mzazi ambaye alikuwa anaumia zaidi, hakuna marefu yasiyo na ncha, nimefunga jalada la utoto, nimefunga jalada la ujinga, naomba radhi kwa haya yaliyotokea", amesema Wema Sepetu.
Wema ameongeza kuwa "Nitakuwa binadamu wa ajabu sana iwapo nitasema sijaguswa, nimejikuta kwa mara ya kwanza nimejali, tangu jana mpaka sasa siko sawa".
Jana kupitia mitandao ya kijamii, zilisambaa video za mwanadada huyo akiwa na mwanaume aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa ambaye alimpost siku za hivi karibuni katika ukurasa wake wa instagram.