Tuesday , 4th Mar , 2014

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga wanaataraji kuondoka nchini kesho usiku kuelekea nchini Misri

Wawakilishi hao wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani afrika Dar es salaam Yanga afrikans wako kambini nje kidogo ya jiji la dare s salaam wakijifua katika uwanja wa bocco beach veteran wakijiwinda na mchezo wa marudiano dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Al ahly Misri mchezo utakaopigwa march 9 jijini Cairo

Katibu mkuu wa timu hiyo Beno Njovu amesema kuwa wamejipanga vema katika kuhakikisha timu hiyo inakwenda kulinda ushindi wake wa bao 1-0 walioupata machi mosi hapa nyumbani na hivyo kuwaondoa na kuwavua ubingwa huo mafarao hao wa Misri

Aidha Njovu ameongeza kusema kuwa katika hali ya kukwepa hujuma na fitna za waarabu hao wamewasiliana na wizara ya mambo ya nje katika kuhakikisha timu hiyo inapata huduma ya maji na chakula kutoka ubarozi wa Tanzania nchini Misri ili isiweze kuhujumiwa kwa njia yoyote ile.