Thursday , 31st Jul , 2014

Staa mkubwa kabisa kutoka Uganda, Jose Chameleone atadondosha bonge la shoo katika Tamasha la 'Tubonge' hapo kesho ndani ya ukumbi mkali wa starehe wa Maisha Club uliopo jijini Dar es Salaam.

msanii Jose Chameleone wa nchini Uganda

Msanii huyu mkubwa ambaye pia yupo katika orodha ya wasanii 10 matajiri zaidi Afrika, atafanya onesho hili sambamba na msanii Vanessa Mdee ambaye anafanya poa katika muziki hapa Bongo.

Mashabiki wa muziki Bongo watapata nafasi ya kusikia Live ngoma kali kutoka kwa Jose Chameleone zikiwemo Gimme gimme, Tubonge, Wale Wale na nyingizo kali.

Kiingilio katika onesho hili la aina yake ni shilingi 15000 tu kwa tiketi za kawaida na 30,000 kwa zile za VIP, Tubonge Concert inakujia kwa udhamini mkubwa wa EATV na East Africa Radio.