Sunday , 8th Jul , 2018

Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Shaaban Iddi Chilunda amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na CD Tenerife ya Daraja la Kwanza nchini Hispania.

Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Shaaban Iddi Chilunda akisaini Mkataba.

Meneja wa Azam FC, Philipo Alando amesema kuwa klabu hiyo ya Santa Cruz mjini Tenerife, visiwa vya Canary imeamua kumchukua mchezaji huyo, baada ya kuvutiwa na mchezaji mwingine wa Tanzania, Farid Mussa.

Alando amesema kwamba ni wiki mbili tu tangu Tenerife imnunue moja kwa moja mchezaji mwingine wa zamani wa Azam FC, winga Farid Mussa ambaye pia walimchukua kwanza kwa mkopo miaka miwili iliyopita.

Shaaban Iddi ambaye atatimiza miaka 20 Julai 20 mwaka huu tangu azaliwe mwaka 1998, alijiunga na akademi ya Azam FC Jumamosi ya Julai 21, mwaka 2012 kabla ya miaka miwili baadaye kupandishwa kikosi cha kwanza.