Television ya EATV kesho itazindua rasmi shindano la Dance 100% kwa mwaka huu. Shindano hilo lenye mvuto na ubora wa hali ya linarudi tena kwa kasi mpya ikiwa ni mara ya tatu mfululizo,shindano ambalo limewavtia vijana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 25 wakishindana kucheza kwenye mashindano haya ya Dance 100% kuwania ubingwa na zawadi ya fedha Taslimu.
Zoezi la mchujo au auditions litaanza Jumamosi ya Tarehe 19 Agosti 2014.kuanzia saa 4 Asubuhi mpaka saa 12 jioni katika viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es salaam.
Mchujo huo wa kwanza utafuatiwa na michujo mingine miwili itakayofanyika Don Bosco Oysterbay na viwanja vya TCC Changombe Tarehe 26 Agosti na tarehe 3 Septemba .Jopo la majaji katika shindano la mwaka huu litaongozwa na mtangazaji maarufu wa Television wa kipindi maarufu cha Nirvana Lotus Kyamba,Mkali wa dansi na mwanamuziki Super Nyamwela na mwanamuziki maaruifu wa Bongo Flava Queen Darlene.
Kwa karne kadhaa maandiko ya hekima yameelezea faida za kusakata Dansi ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya vioungo.Hata tafiti mbali mbali zimelezea faida za kucheza muziki ikiwa ni pamoja na kuondoa msongo wa mawazo na kuongeza uhai wa kuishi.Hivi karibuni tumesikia faida nyingine ya kucheza dansi mara kwa mara inatufanya kuwa watanashati na kutoa ajira kwa makundi ya vijana na watu binafsi.
Television ya EATV inawaalika mashabiki na wapenzi wote wa Dance 100% na wapenzi wapya kuja na kushuhudia ubunifu wa kucheza dansi kwa pamoja choreography na sanaa kwa ujumla.
Hakuna kiingilio katika shindano hili kuanzia mwanzo mpaka mwisho,hivyo unakaribishwa kushudia vipaji vipya.Washiriki na watazamaji hawatakiwi kuwa na wasiwasi ya kwamba hautatumia kile ulichojifunza hapo baadae kwani unashauriwa kuitumia hiyo fursa kuipa changamoto akili yako
kwani itachochea kuunganisha akili yako katika ulimwengu wa ubunifu na sanaa.
Tukutane sote pale viwanja vya Don Bosco Upanga Upanga kuanzia saa 4 asubuhi kwa ajili ya msimu mpya wa Dansi 100%.