Friday , 15th Jun , 2018

Nchini Kenya mwanaume mmoja aliyejulikana kama Mike Otieno (47) ameuawa kwa kunyongwa na wananchi wenye hasira kali kwa kile kilichodaiwa ametekeleza mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake.

Otieno anasemekana alikuwa na mwanamke huyo aliyejulikana kama Achieng katika klabu moja ya usiku huko Kondele siku ya Jumatano usiku kabla ya kurudi naye nyumbani majira ya saa nane alfajiri.

Wakazi mji huo waliamka mapema asubuhi na kukutana na mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa vipande vipande, ukiaminika kuwa ni wa msichana anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 19 na kuwekwa kwenye begi.

Kwa Mujibu wa Polisi Kituo Kikuu cha polisi cha Kisumu wamesema kuwa mashuhuda wanasema mtu huyo alikuwa amenyongwa alfajiri ya Alhamisi baada ya mlinzi wa usiku walipotoa taarifa juu ya jaribio lake la kuutoa mwili wa mpenzi wake kutoka nyumbani kwake kwa kutumia begi.

“Mlinzi amesema alisikia kilio cha kuomba msaada kutoka kwenye nyumba ya mwanaume huyo kabla ya vilio hivyo kumezwa na sauti kubwa ya muziki muda wa saa kumi na nusu alfajiri,” amesema kamanda  Meshack Kiptum.

Ameongeza kuwa mlinzi huyo alishtuka mnamo muda wa saa 10 alfajiri mwanaume huyo alipomwomba afungue geti ili rafiki zake waingie na kumsaidia kuhamisha mzigo muhimu.