Friday , 15th Jun , 2018

Mbunge mmoja nchini Urusi anasema kuwa wanawake hawatakiwi kufanya mapenzi na wageni wakati wa kombe la dunia huku ambapo ameeleza kuwa watoto wanaozaliwa huwa na rangi tofauti kitu ambacho kinapingwa vikali ncini humo.

Bi. Tamara Plentyova ambaye pia ni Mbunge wa chama cha Kikomunisti na Mkuu wa kamati ya familia, wanawake na masuala ya watoto bungeni, amesema  kuwa hata iwapo uhusiano huo utasababisha kufanyika kwa harusi, wanawake au watoto wao watachukuliwa na mwanamume huyo ambaye atakuwa raia wa kigeni.

''Hata wakiolewa, watawachukua, halafu watashindwa namna ya kurudi. Baadaye watakuja kwangu, wasichana wakilia kwamba watoto wao wamechukuliwa" amesema Bi. Pletnyova akiwa katika kituo cha habari Govorit Moskva.

Hata hivyo ameongeza kwamba wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya 1980 mjini Moscow walibakia kuwa wanawake wajane.

''Ni vyema iwapo ni mtu wa rangi inayofanana na yako lakini iwapo ni mtu wa rangi tofauti basi kunakuwa na shida. Ni muhimu kuwa na watoto wetu'' ameongeza.

Warusi wenye ngozi nyeusi hadi leo hukabiliwa na maswali mengi ya ubaguzi wa rangi katika taifa ambapo chini ya asilimia moja ya idadi ya watu ni wana ngozi weusi.