msanii Weasel wa nchini Uganda
Katika mahojiano yaliyofanywa na msanii huyo ameelezea kuwa anamfagilia mno askari polisi wa kike nchini humo anayeitwa Judith Nabakooba kutokana na utendaji wake wa kazi.
Weasle amemwagia sifa askari polisi huyo ambaye ni msemaji wa polisi akimwelezea kuwa ni mtu mtaratibu na msema kweli asiye kuwa na makuu katika utendaji wake wa kazi.