
Washirika wa Marekani wamekasirishwa na hatua ya rais Trump ya hivi karibuni kutoza ushuru vyuma na bidhaa za aluminium , hatua inayozua hofu ya kuzuka kwa vita vya kibishara.
Haijulikani iwapo makubaliano ya pamoja yatawekwa hadharani baada ya kukamilika kwa mkutano huo ambapo tofauti hizo zilionekana hadharani kabla ya kuanza kwa mkutano leo.
Tofauti kati ya Trump na viongozi wengine sita ni zaidi ya tofauti za kibishara zilizopo- zinashirikisha hali ya tabia nchi, uhusiano na Iran na mgogoro kati ya Israel na Palestina.