Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Seif Rashid.
Akiongea na East Africa Radio, Meneja wa Huduma za Kliniki wa Chama cha Afya ya Uzazi nchini Tanzania (UMATI) Dkt. Saili Mbukwa amesema katika kila wanawake 100 wanaokwenda kupima, wanawake sita wanabainika na kuwa na saratani hiyo hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na vijana kuanza mahusiano wakiwa na umri chini ya miaka 18.
Dkt. Mbukwa amesema hali hiyo inatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanawake kuwa na wapenzi wengi, na hivyo kupata maambukizi ya saratani na kuongeza kuwa kwa sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wanafunzi kati ya miaka 10 hadi 18 ili kuepuka na saratani hiyo.