vyao vipya vya kazi.
Mabalozi hao ambao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam, Mh. Suluhu amewatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais.
“Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” amesema Mh. Suluhu
Kwa upande wao Mabalozi hao wamemuahidi Makamu wa Rais kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.